lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

amen - rapcha ft lady jaydee lyrics

Loading...

hebu tazameni, matendo ya mungu yanavyotisha
amefanya mengi makubwa ya kustaajabisha
marafiki leo wana upendo kesho umekwisha
ila upendo wa mungu hauwezi kuisha

naamini neno lako linaishi forever
utandawazi hauwezi kubadili dhambi ikawa haki, never
umenifikisha sehemu ambazo wala sikuwahi kuzifikiria
sifa zako nitahadithia

unaniepusha na maadui
unanilinda na mabaya ambayo hata siyatambui
mungu uliye hai
hata mimba zilizotokea kwenye mazingira ya dhambi, watoto umewapa uhai

na kama pumzi unanipa bure
sasa kivipi tamaa ya pesa initenge na wewe
nashukuru kwa kunileta hii sayari
milele nitakuamini mungu wa kweli.. amen

chorus:
amen baba amen
upendo wako, huruma yako amen
wema wako , utukufu wako , amen
amen baba amen
umenipa maarifa
umenipa uhai umenipa mali
hata nacho kipaji siwezi sema sijaridhika
umenipa kile ulichonipa hukunitupa
nani sitaki juta baba, nasema amen

verse 2

glory to god, utajiri mkubwa ni furaha
mungu anaweza akubariki mpaka ukashangaa
niwapo kwenye njaa nik*mbushe
kuwa ndege hawalimi, hawavuni ila hawakosi chochote

nilipotoka usiache nik*mbusha
nipe hekima nisitamani magari nisiyoweza kuyaendesha
niishi kwenye ukweli nidumu
maana uongo hauishi milele na unaua fasta zaidi ya sumu

pia asante kwa kunipa bidii
nnapokuomba haujibu haraka unajibu wakati sahihi
una hekima inayoshangaza dunia
watu hata tugombane vipi tunashare mvua na jua

nijalie nisilewe sifa
nik*mbuke siku za uhai w*ngu zinahesabika
hivyo nikuabudu nikiwa kijana
nawe utaniweka juu kwa baraka leo zaidi ya jana

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...