kipi sijasikia - prof. jay lyrics
[verse 1: prof. jay]
ah
niliacha kazi nifanye muziki wakatabiri nitalost
wengine wakanishawishi tuloge kuondoa mikosi
nakomaa na muziki ingawa jua la utosi
naamini wote tunapita na kamwe maiti haijioshi
jina langu lishatumika sana kutajirisha watu
nyota ndogo alishasema kuna watu na viatu
bunduki haiui watu ila watu ndio wanaua watu
dunia kama jalala tazama kwa jicho la tatu
ni saa mbaya watu wanahusda na roho mbaya
tunawaita watakatifu k*mbe ndio ma vampire
yalisemwa mengi demu w*ngu alivyotoroka
ni fundisho tosha na changamoto kwa mwanachoka
nimepita mengi mitihani ya kila namna
ndio maana mi sishangai wakiniita mbeba lawama
washkaji wengine fake kwenye deal hawakujui
wanadhani kila jogoo akiwikia ni asubuhi
riziki hamuwezi iziba labda m’taichelewesha tuu
m’nakesha m’nishushe mwenyezi ananipaisha
kote milikobana kidume ndio natusua
m’nanijua, nakamua, roho za w*ngu zingaungua
platnumz
[chorus: diamond platnumz]
oh
unaehuk*mu ni wewe
mwenyezi mungu naomba unilinde
kwenye hii vita milele
basi nishike mkono nishinde
unaehuk*mu ni wewe, ah
mwenyezi mungu naomba unilinde, ah
kwenye hii vita milele
mwanachoka dama nishinde
[verse 2: prof. jay]
walishazusha nimekufa
eti nimepata ajali
washindwe na walegee
mwenyezi niepushie mbali
wakasema nina ukimwi kwa kuwa nilikonda ghafla
wanataka kunizika mzima kabla sijafa
waliosema nina ngoma wengine tushawaf*kia
wanaomba nife leo naamini watatangulia
mama pumzika pema, daima tunakulilia
na bado wanachonga sana but man, the king is here
daima m’taji w*ngu ni nguvu zangu mwenyewe
simwamini m’tu kamwe naijamini mi mwenyewe
hata nikinywa maji wanadai nakunywa pombe
mi sijali
i knock them hard, mwana lizombe
bado tu napambana kibarua kisiote nyasi
daima sitawadhuru wale wote walioniasi
nikika kimya msidhani sijasikia
sio bahati sio ngekewa ni sauti iliyobarikiwa
holla
[chorus: diamond platnumz]
oh
unaehuk*mu ni wewe
mwenyezi mungu naomba unilinde
kwenye hii vita milele
basi nishike mkono nishinde
unaehuk*mu ni wewe, ah
mwenyezi mungu naomba unilinde, ah
kwenye hii vita milele
mwanachoka dama nishinde
[verse 3: prof. jay]
mungu walaze pema waliosemwa wakajiua
ingawa wote tunapita naamini maisha ni hatua
maneno ya watu sumu, yanaponya na yanaua
please nipe ujasiri mpaka siku ukinichukua
wape nguvu wale wote waliokata tamaa
maneno y*n*leta hila na mzozo kwenye mitaa
wanahesabu mabaya tuu na mema hawayaoni
wanakuchekea machoni, wanakuroga moyoni
wanacheka chini chini wakati una msiba
wa kwanza kukutangaza kwa watu ukiwa na shida
wanatamani wapangue kila mola alichopanga
wanatangaza amani huku wameficha mapanga
[chorus: diamond platnumz]
(eiih) oh
unaehuk*mu ni wewe (oh…eh)
mwenyezi mungu naomba unilinde (oh, ni wewe baba)
kwenye hii vita milele (eh)
basi nishike mkono nishinde (oh, ni wewe baba)
unaehuk*mu ni wewe, ah
mwenyezi mungu naomba unilinde, ah (oh, ni wewe)
kwenye hii vita milele
mwanachoka dama nishinde
[middle 8: diamond platnumz]
tai
mi maneno nishazoea (uh huh)
ndio maana sijali wanapo ongea (uh huh)
eih
wanasemasema mengi, mengi, mengi
tu hili mabaya (uh huh)
oh, mi nimeshazoea (uh huh)
ndio maana sijali wanapo ongea (uh huh)
hey
wanasemasema mengi, mengi, mengi…
[outro: diamond platnumz]
iye, iye
oh hey, yeah
oh yeah, yeah
oh hey, yeah
iye, iye
tuturururu
tuturururu, yeah
tuturururu, eh heh
eh heh
eh heh
eh heh
eh heh
Random Song Lyrics :
- glock 9 - donnie darko lyrics
- aftermath (alright remix) - area: 508 lyrics
- pirmkursnieces - uve šļams, slenderzutis lyrics
- качели. часть 2 (kacheli. part 2) - centr lyrics
- fake woke - weezle lyrics
- triple x lullaby (トリプルエックスの子守唄) - z. konketsuji lyrics
- koek en ei - donnie (nl) lyrics
- kris - d'shaun lyrics
- #ff4 - d. ace lyrics
- block b - bts gang lyrics