sikiliza - ngwair lyrics
[intro: ngwair & mwana f.a.]
woo!
ngwair na f.a., holla
binamu
east zoo y’all (yeah)
na [chris paul]
ah, yo jide
(?)
[chorus: lady jaydee & mwana f.a.]
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hatakama sijamaliza, yeah
aah, sikiliza what?
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hatakama sijamaliza, yeah
aah, sikiliza
[verse 1: ngwair]
yow
nyie mademu ninyi, nisikilizeni kwa makini
mimi hivi kwanini mnakuwa hamniamini? (yeah)
najua nyie yaani mna nguvu zaidi ya sisi
mwanaume kwa demu ni kama mfupa kwa fisi (uh*huh)
sina nia ya kubadili maadili, sio
nnacho pinga nyie kushikwa masikio (yeah)
sema tu hamjui umuhimu wenu
ila leo nitawaambia tu ila iwe siri yenu (what?, nitasema)
mi mwenyewe naenda club kila wiki (kila wiki)
haina maana huwa nafata tu muziki (wa kazi gani?)
mkiwa wachache huwa naona hapalipi
hata niwe na hela vipi, na rundo la marafiki (nachukua time)
vijijini ni asilimia tisini maskini, starehe yao ni pombe na ninyi (yeah)
sasa mpaka lini mtakuwa mnanyanyasika na kudharaulika?
au wenyewe mmeridhika? (?)
kuolewa ‘mna haki wala msiitе bahati (what?)
we unadhani ‘wanangu mi ntalea na nani?
sema tu wеngi wenu ni vicheche, j*po sio moto
hakuna asie ogopa (?), yeah
[chorus: lady jaydee & mwana f.a.]
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hatakama sijamaliza, yeah
aah, sikiliza what?
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hatakama sijamaliza, yeah
aah, sikiliza
[verse 2: mwana f.a.]
mfano mimi [siamini] kabisa mtungi
ukiacha mabinti, sio mi nelly, sio mirungi (sio mirungi)
ila nakosa imani nikiwaona mnajigonga
yaani hadhi yenu inashuka, ki msimamo mnapo yumba
mmekosa nini?, kinachofanya msijiamini
au mwalimu wenu kipofu, msemo nanyi mnaamini?
msichimbe madini, sawa!
ila sio wote muwe wafanyakazi wa ndani
hesabu hazipandi so ‘ni ngumu kuwa rubani
ila ‘j*po karani na imani haishindikani
big up kwa my mommy (mommy)
wote ambao kompyuta imelala kichwani
sisemi mlee wanaume kama mabinti ila mnavyo jitosheleza machaguo yanaongezeka, hamuoni? ‘basi someni
kama uliishi vibaya kwa wanao ‘jirekebishe
wenye upeo mdogo ndio daima wanakuwa vicheche
kuolewa sio lazima, j*po inaongeza heshima, ina hadhi yake
hawatojali mke wa kigogo au wa mkulima
na ole wenu msiopenda kutafuta vyenu
mnatamani tu vya wenzenu, ndio maana huwa mnamegwa na wazee umri wa babu zenu
nieleweni, jikazeni’ msipo komaa waume zenu watawaletea vicheche ndani, niamini
binamu, b’
yeah
[chorus: lady jaydee & mwana f.a.]
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hatakama sijamaliza, yeah
aah, sikiliza what?
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hatakama sijamaliza, yeah
aah, sikiliza
[verse 3: ngwair]
kingine ‘mnapenda sana vya kupewa
ndio maana wengi wenu mnaishia kuchezewa
mna megwa, mna achwa na hata mkiolewa (yeah)
ndoa inajaa visa na kuonewa
mfano ngwair narudi muda nnaotaka
na ukiniletea kibezi ti asubuhi talaka (kwenu)
sinajua huna kitu zaidi ya begi lako (mf*ko wa rambo)
ila nisinge dhubutu endapo nyumba ni yako (uh*huh)
najua hamuwezi kwenda haja ndogo mmesimama
ila mna uwezo wa kufanya kila sisi tunachofanya (yeah)
hata kuwa rais mwanamke pia ana haki mradi tu uwe na vigezo, wanaume tunapata wapi? (uh)
kama kusoma, wote ruksa kusoma
bado biashara hata ufundi wa kushona
wenzenu wachache bungeni, si mnaona?
hata kuimba imbeni tu ‘msione noma
(?) stara, ray*c, yeah
mnataka kuendesha prado kama lady jaydee (komando!)
amini wote tumezaliwa watupu na kupata hutokana na juhudi tu za mtu, yeah
holla!
[chorus: lady jaydee & mwana f.a.]
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hatakama sijamaliza, yeah
aah, sikiliza what?
kama ni demu sikiliza, niskize mi
kama una swali uliza, niulize mi
hatakama sijamaliza, yeah
aah, sikiliza
yeah
(instrumentals)
Random Song Lyrics :
- the battle of all - richard miller lyrics
- à ma place - emma daumas lyrics
- pianito - los pericos lyrics
- i. bad mood - jisaiah lyrics
- we only read the headlines - lazyboy (tv) lyrics
- payday lyrics - nifti noel lyrics
- olhe menina - nelio guerson and carlos guerson lyrics
- illusion - poor moon lyrics
- introvert - superjoint ritual lyrics
- suba la mano - oliver ontañon lyrics