mungu yuko wapi - nay wa mitego lyrics
hawa hawa hawa hawa
hawa hawa hawa hawa
nilizaliwa peke yangu
na nitakufa peke yangu
muamini mungu wako
nibaki na imani yangu
kama kweli kuna mbingu
basi nina njia yangu
sio baba sio mama
nitakwenda peke yangu
mungu hamtupi mja wake
imeandikwa kwenye vitabu
mbona shetani ametawala
na waja wanapata tabu
hivi kweli huyu mungu yupo?
na huu mchaf*ko
uliyokataza yametawala
hivi kweli we mungu upo?
wenye roho mbaya mungu ni wewe umewapa hela
wana makosa kibao na bado hatuwaoni jela
kuna hawa viongozi makatili na madictator
wanatesa watu wanauwa watu
sababu ya madaraka wanajiona miungu watu
baya zaidi hawafi haraka watu wenye roho mbaya
mungu ni kweli upo na unayatazama haya
hivi ni wewee, ni wewee
hivi ni wewee
sasa mbona upo kimya
hawa hawa hawa hawa
hawa hawa hawa hawa
hivi mungu yuko wapi?
hivi mungu yuko wapi?
hivi kweli mungu yupo?
hivi kweli mungu yupo?
ninae muabudu mimi
sio mnaemuamini nyinyi
najua tuko tofauti
kuanzia imani mpaka dini
na sitoshangaa
msipoelewa naongea nini
maana mi mwenyewe siеlewi
mnashangaa nini
pumbavu nyinyi wajinga nini?
mnateswa mnanyanyaswa
mnangoja nisemе mimi
eeh mungu baba hivi kweli unaona?
hivi anaewapa hela mashoga ni mungu gani?
wanaosagana wana roho gani ya imani
mbona dada yangu ameokoka ila anakufa maskini
wakati wenzake wadangaji anawapa hela kwa nini
au ushakula kona shetani ametake over
manabii wa uongo wamejaa kila sehemu
tunalewa nao tunashare nao mademu
sadaka za watu wako ndo zinawapa wazimu
wanatumia jina lako
wanaponya kwa nguvu za giza
ufuska mauaji ukatili uliopitiliza
hivi kweli mungu upo ndo swali nnalojiuliza
hivi ni wewee, ni wewee
hivi ni wewee
sasa mbona upo kimya
hawa hawa hawa hawa
hawa hawa hawa hawa
hivi mungu yuko wapi?
hivi mungu yuko wapi?
hivi kweli mungu yupo?
hivi kweli mungu yupo?
wanaokesha kwa waganga wanafanikiwa kwa spidi
wanaokesha kwenye ibada maisha yao duni
hivi ni wewee, ni wewee
hivi ni wewee
sasa mbona upo kimya?
hawa hawa hawa hawa
hawa hawa hawa hawa
mungu uko, mungu uko
where are you?
uko wapi, uko wapi?
(free nation, mr lg)
Random Song Lyrics :
- i could never - jourdan brothern lyrics
- sleep walk - benson & bruno furlan lyrics
- космос (space)* - кишлак (kishlak) lyrics
- wicked inna raq 2 - lil nuu lyrics
- cities and plans - north of america lyrics
- tsla - larussell lyrics
- what to do ? - kierre lyrics
- take my love - good shape lyrics
- poet turned rapper - nour rakha lyrics
- summer rain - jasiah lyrics