amkeni - nay wa mitego lyrics
raisi
listen to me
nitakachokiongea unaweza niona sio mzalendo
zalendo zalendo gani
nchi inaendeshwa kimagendo
wengine mwisho wa wimbo huu mtasema mimi mchochezi
kila kitu kipo wazi mama yenu *n*lea wezi
ndiyo anafuga wezi hapa kikubwa dua
hata report ya cag hakuna aliyechukuliwa hatua
yani kodi kila sehemu na bado mnakopa daily
bandari mme muuzia mwarabu na mkataba ndo wamilele
najiuliza why mungu ulimchukua john mapema
ulimchukua tujifunze au tupate kuhema
huu mtihani haki ya mungu mimi nakosa cha kusema
kazi yako haina makosa ikikupendeza chukua na hawa
media za bongo zimestuck hazina tena ubunifu
hazikuzi presenter wapya zinaangalia nani maarufu
mh
na hao maarufu sasa hao machangudoa
mwenye kisu kikali huyo ndo atakae mng’oa
ah
amkeni nyinyi hakuna elimu ya bure
ninachojua mimi elimu ni gharama
siku zote nachoamini cha bure akina maana
wanatupa elimu mbovu ya bure isiyo na maana
na ndo maana siku hizi tunawasomi wajinga sanaa
pro ya mama ni kubwa kuliko utendaji wake
mabango kila kona
wanamdanganya ndege bora kuliko ongezeko la mshahara
wanamshauri aongeze ndege mashirika yanaendeshwa kihasara
ukiwachukua viongozi wetu wakaiongoze marekani
na wamarekani waiongoze tanzania
baada ya miaka mitano marekani itafulia
kwamba watarudi kuomba msaada tanzania
nishatafuta kazi elimu yangu nikakosa
nikatafuta kazi ya mshahara mdogo nikakosa
hata ya mshahara wa chakula bado nao nikakosa
nipo na vyeti nangoga miujiza ya mwamposa
tatizo wasomi wengi na walo fanikiwa hawapendi siasa
wajinga ndo wanakimbilia
tunapata viongozi wajinga uchumi umayumba
bongo akili ndogo inaendesha akili kubwa
viongozi ni panya road walio vishwa suti
na sisi walipa kodi tunawapigia salute
nchi imejaa migodi ila tunaongoza kwa dhiki
wanatuuliza mbona atuogi na maji walikata wiki
nyie wajinga sijawatusi ila nyie ni washenzi
na mama ikikupendeza kuhusu mkataba wa bandari
usiishie bara peleka na zanzibari
mnauza twiga mzigo wanatupanga mpaka basi
wabunge kututetea na ukimya mmepaki basi
nguvu kubwa inayo tumika k*mpamba mtandaoni
na kwenye media ila huku mtaani hakubaliki na pia hauziki
endeleeni na ten zenu zakupeana kila wiki
na bunge lenu la mchongo ,spika wa mchongo
limebaki jina la bunge na vikao vya ccm
aya tuache masiala turudi kwenye ukweli
hivi tunapo elekea tunafaulu hama watu wanafeli
miaka miwili tu ilipita tuliishi kwa nguvu ya buku
na ilo buku unachagua unga kilo au mchele nusu
na sasa mzunguko wa bei ni zaidi ya mara tatu
unga kilo buku mbili na mchele ni buku tatu
hapa tu namk*mbuka alisemaga ntamk*mbuka
okay
tuachane na hilo kuna kasumba imezuka
sipendi unafki na uchawa
simlisema haki sawa
ona sasa akikosolewa mnaleta mambo ya jinsia
haitoshi kwa wanao kosoa na kesi mnawafungulia
nawaona tu mnapotea na wakati mnajua njia
aah
mnauza twiga bado mzigo anatupanga mpaka basi
wabunge kututea na ukimya umebaki basi
amkeni nyinyi hakuna elimu ya bure
nachojua mie elimu ni gharama
siku zote nacho amini cha bure akina maana
wanatupa elimu mbovu ya bure isiyo na m,aana
ndo maana siku hizi tunawasomi wajinga sana
Random Song Lyrics :
- rudý květy - earth (cze) lyrics
- 3:00 - eso ent lyrics
- i want to believe - rand (itsjustrand) lyrics
- ballsack's plan - lil ballsack lyrics
- birthday - rj keeper lyrics
- moonlight - gris anthracite lyrics
- 3. shabolda (demo 2203) - highswag lyrics
- feel - büyük ev ablukada lyrics
- prouver - rémy lyrics
- drowned maid (2010 version) - amorphis lyrics