lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

gwiji - mwanafa lyrics

Loading...

nyoshi;

aaah mwanafa,nkoyiii
omeki okangami,wewe ni gwiji wa magwiji/
asiyekubali,aumbe dunia yake/
lakini mimi nyoshi el saadat nakuchukuliaga kama mobutu sese seko kuku ngbendu wa zabanga,le martial bosomba,seskuule,hahahaha
never end,never lose
mwanafa, légende légende légende

falsafa;

naota ndoto hazina rangi,naamka n*z*paka/
watoto wa kiswazi huwezi ukatuwekea mipaka/
mungu ndio ametaka,jongoo kawa nyoka/
hakuna kiunzi hatuwezi ruka/
tushasuk*ma sana milango iliyoandika vuta/
niamini na inafunguka/
mbwa mkali usikatize,wahuni tunapita/
tunayavuka kwa kamba madaraja yaliyovunjika/
mungu wetu halali,wala haendi likizo/
hatuachi k*muomba na anafuta matatizo/
yakija tena naomba tena na mungu anayafuta tena/
mioyo yetu ipo safi,safi ile kinoma/
kifo kiniue au maumivu yanikomaze/
yote sawa ila ujinga usinipumbaze/
kila kiumbe ana njaa yake,moyo na tamaa zake/
mbwa mpumbavu ndio anaweza bwekea ndege/
maua;

waiteee wamuone gwiji wajigambe/
waite waite waje wamuone gwiji wajigambe/
we hayaa x 2

falsafa;

mi ni hustler babe that’s what i do,i hustle/
shida hazikwepeki zipo kukupima muscle/
zikutoe macho,zikutoe jasho/
zikupe akili na zikuandae kwa kesho/
jikaze mwana usichukuliwe mateka/
ka unaachana na dunia we ndio uandike talaka/
ukiomba mafanikio fahamu yanakuja na wivu/
havitengani havikai mbali,kidevu na ndevu/
dunia haitasimama ukigoma kutembea nayo/
sio magumu ka ku’cl!ck link kwa bio/
kakamaa nakupa moyo/umegusa tu b*tton siyo/
kuwa mpambanaji kama binamu yangu suyo/
huu sio mziki wa mafala,ni mziki wa mataita/
unakuweka kitako na chaki unakufundisha/
una’feel the passion,zaidi ya telemundo/
mapanchi mengi hata touch akizima mdundo/
bye bye

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...