lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

tuambie - mikka lyrics

Loading...

ona sasa vile wanatuchanganya
wanasema ati kazi kwa vijana
lakini bado hizi kazi hatuj-pata
waliyo ahidi hawajafanya
na kwa habari wajigamba
lakini jua pia sisi ni wajanja
tunaona yote ila twanyamaza
twaachia maulana

tuambie
jeh twasonga mbele au twarudi nyuma
tujenge nchi yetu iwe bora
au bado turidhike na madrama
tuambie
ni siku gani tutaishi na salama
hadi lini tutanyimana baraka
au bado mikono mtazikaza
tuambie

kura zikikaribia twapatana
siku zingine ofisi hamtakanyaga
mteja wanambari hautawahi mpata
ni rahisi kusahau jana
jeh bila sisi hizi cheo mgepata?
pia sisi tunaomba kujipanga
tufurahie kila mtu madaraka
na kesho yetu tuachie maulana

tuambie
jeh twasonga mbele au twarudi nyuma
tujenge nchi yetu iwe bora
au bado turidhike na madrama
tuambie
ni siku gani tutaishi na salama
hadi lini tutanyimana baraka
au bado mikono mtazikaza
tuambie

tuambie
jeh twasonga mbele au twarudi nyuma
tujenge nchi yetu iwe bora
au bado turidhike na madrama
wakubwa tuambie
ni siku gani tutaishi na salama
hadi lini tutanyimana baraka
au bado mikono mtazikaza
tuambie

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...