lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

zamani july (interlude) - ghafla lyrics

Loading...

turudi miaka ya tisini sitaki kuishi nyumba ya udongo tena
tabu zote sidhani zina uzito mi siwezi beba
nidhamu nyingi za woga zimegharimu washkaji watu vena
siku hizi kuhusu mitaa marapper wengi huwa hawafanyi tena
mziki sio biashara njema
mameneja ndo wanaogawa tenda
kusikika tu hewani ni mtaji kurekodi sio ishu tena
kuhusu madj’s labda tuseme haiendi bila pesa
zamani july haikuwa ubinadamu kazi sana nature
kwa kauli ya hapa kazi basi siku hizi mziki mzuri pesa
mademu wanauza uchi..tenda
washkaji wananunua..vyema
inakuwaje galla boy mkenya
ni uzalendo umekushinda au mapichapicha hili game sinema
tukiacha unafki kiukweli hili game sidhani
wanaoweza ndo wengi wanafanyia harakati
vipaji vinafia mtaani wengi waliotoboa wamewekeza pesa
bonge la entertainer show anahema beat hawezi kwenda
machizi wengi ndo sisi tunaowakilisha vyema
kuhusu hizi kiki ndo u*hit ndo ngoma iweze chezwa
ukiwa unaweza huwezi weka heshima rehani tena
upige picha za uchi ndo utoke vipi unaweza zena?
kiki zinaandikiwa script unataka u*hit je unaweza cheza?
ndo maana wengi ukiwapa beat hawana kitu zaidi ya one two
watacheka kidogo zima mziki naimba kavu
wataimba mstari mmoja mstari wa pili ataanza kucheka tu
atamgeukia dj twenzetu weka ngoma yangu
i miss you mama,duniani kuna mambo
wakinianika kwenye ibada sijakamilika tu kama wao
tatizo ni binadamu akishajua madhaifu yako
rafiki wanauza siri na mafanikio ndo chanzo
hadi wanaume wanauza mwili nashukuru mungu sijambo
magonjwa yameanikwa njiani na wenye tamaa ndo chambo
nahitaji amani ya maisha hatuna uadui nipe tano
nahitaji upendo huenda ikatupa hiyo amani kwa mfano
nahitaji shibe ya halali asiumie mwingine wa kandoo
na binti niliyempenda alisema hapa ni pesa yako
movie kila week na ulipe bili ya viwalo
hiyo sio aina ya mademu anaowapenda sam misago?
u*shine ka mimi,u*ride ka mimi
au useme ka mimi
namuona yule pale
zamani july alikuwepo mkali nesta marley
kama hauwezi ni hauwezi tu
zamani july,kuuenzi huu mwezi iwe sabato july

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...