naishi nao - ghafla lyrics
“naishi nao” * ghafla
intro
(anhaaa haha haha,oh my god)
sii sii sii
yeaah,right
mmmh,a city
g.h.a,,i’m blessing..aah
(its chris beat) lets go
aaah,right,,yeaah,,aah,right,,aah
verse
inashangaza wasiotupenda tunang’ang’ana kuishi nao
nimezunguka kutafuta upendo na sikujua naishia nao
mademu wengi niliolala nao sikuwahi kuamka nao
laiti ningewapa moyo w*ngu w*ngeamua kuishi nao!
leo ningebaki tu na figo na sikujua lengo lao
labda w*ngechukua uhai w*ngu maisha yangu wakaishi nayo
adui zangu hawapo mbali ndio najua naishi nao
zaidi ya mola nani anilinde inabidi nishinde nikiishi nao
wanasiasa tunaishi nao
wanapokaa mnajua ni mbali ni ngumu kufikia ahadi zao
ndo maana huwa siwazingatii nimeshakosa imani nao
nao polisi tunaishi nao
bado hatuvuti hewa kwa raha j*po moshi tunaishi nao
bado tunapigwa roba ya mbao
maana vibaka tunaishi nao
nawaambia wanangu kaeni mkao
chochote kinaweza kikatokea si mmeshaona umeme wa mgao
hakuna anaejali hata mkiondoka wao wanaangalia matumbo yao
na ndugu zetu wapo south
maisha yao sio kitu tena mbele ya randi na hizi pound
watoro wa nchi watarudi maiti na mtaskia itavyo sound
siku hizi za mwizi hazina round
arobaini atazikuta tukishamzika underground
sijawahi ku sound ka underground j*po underground naishi nao
nimeelewa na mizigo mizito ipo mabegani naishi nayo
nilipopita nimeacha alama waache washindi wafuate nyayo
wanangu wamenizunguka muda wote naishi nao
malaika wapo pembeni muda wote naishi nao
mtoto wa mungu ni ka napaa wanashangaa hawaoni mbawa
mapresenter naishi nao
hawa djs naishi nao
ila utafikiri ka hatujuani ukiskiza media zao
siku hizi nacheka halafu imeisha sitaki kujua habari zao
mziki w*ngu najua ni dawa umewaponya watu kibao
maisha yangu najua ni somo mkijifunza mkaishi nayo
haya matunda kula peke yangu huwa inaniumiza mara kibao
natamani ningekuwa na wanangu tuliopambana kuchuma nao
moyoni mw*ngu bado mnaishi niseme niwazike naanzaje how
shabiki zangu naishi nao
nipo nao huku mtaa hawapendi kuona napiga miayo
hivyo wanavaa tu mtaa cash wakinipa naishi nayo
mama zangu naishi nao
wamenilea ka mwanao hivyo na wanao naishi nao
baba zangu naishi nao
si unajua inakuwa kiume ukizingua ni vibao
siku hizi tunatinga vizibao na dada zao tunaishi nao
tupo ghetto ila mademu wa kishua tunaishi nao
ngumu kututenga sisi ni ukweli maana ukweli tunaishi nao
roho nyeupe sijui ni lini nitaondoka sitoishi nao
hakuna cha kudumu milele haya maandiko naishi nayo
hampendezi aliye juu hivyo machoko siishi nao
tukikutana iwe kwa upendo j*po kwa beef nitaishi nao
mi ni mtaa mi ni g mi nitabaki mkali wao
hivyo ukiwaona waambie wasiogope kivyovyote nitaishi nao..daamn
bridge
coz im blessing
(namna tumebarikiwa au sio)
coz im blessing
(mungu ni mwema kila saa)
coz im blessing
(mungu anajua lini na wapi,nani na nani)
coz im blessing
(toka mtaa block za udongo)
kivyovyote nitaishi nao
(mpaka kwao)
kivyovyote nitaishi nao
(kwahiyo kivyovyote nitaishi nao)
kivyovyote nitaishi nao
(hakuna cha kuhofia hakuna cha kuogopa)
coz im blessing*3
(mungu ni mwema zaidi au sio)
coz im blessing
(goes by the name g.h.a.f.l.a represent muzik tanzania
waambie wasiogope kivyovyote nitaishi nao)
nitaishi nao nao nao
(yaah,mungu mbele nyuma wao..a city)
Random Song Lyrics :
- leonardo da vinci - loyalkidx & daanitr lyrics
- big boo's haunt - rossanto lin lyrics
- calm down! - boikongpop lyrics
- immobile poets - jasper project lyrics
- i'm autistic i don't get social cues - bj connolly lyrics
- this will all end in tears - bryan dunn lyrics
- 94a9 - high hi lyrics
- cunt wednesday - fiveskin lyrics
- птичка (birdie) - holyweed lyrics
- the club / sorry - juice wrld lyrics