mwanangu - fid q lyrics
[intro]
uh
(?)
uh
uh, yeah
(?)
[verse 1: fid q]
mwili wake utang’aa madini ‘kama ngozi ya papa king
na mke wake atamthamini hata kama kwao ni masikini
mfano wa msimamo aliyo nao ni wakijahidina
na anataka awe mgumu kama rapa ‘kalapina
akupe hekima, busara na heshima pia
baba wa taifa yu peponi, ‘usilie mama maria
mwanangu hunijia ndotoni na ndio mambo ambayo huniambia
mwanangu hunijia ndotoni na ndio mambo ambayo huniambia
akienda kwa ndugu zake ‘hatojisikia yupo nyumbani
sababu baba yake ashaf*kuzwa ‘kosa nilisahau kusuuza sahani
nikatengwa na ndugu na kusaidiwa na mtu baki
upendo wa mungu, mwanadamu aliye na moyo safi
moyo usio kinai, moyo upendao, mwanangu
moyo huu babaangu hana ndio kisa ugomvi na mamaangu
hili songi linamhusu mwanangu ‘na ndio mambo ambayo huniambia
hatochezea elimu ‘ambayo (?) itajenga maisha
w*ngapi walisharusha stimu?
ndio maswali anayo niuliza
siku yangu itapofika nani na nani atanisalia
na w*ngapi watakao nizika
watao nisamehe madeni ‘ambayo ni mengi yasiyo hesabika
mwanangu ananiuliza…
[chorus: banana zorro]
kila siku ndotoni
mwanangu ana nijia
kila siku ndotoni
mambo mengi ananiambia
kila siku ndotoni
mwanangu ana nijia
kila siku ndotoni
mambo mengi ananiambia
[verse 2]
hatopenda kuishi ki*boss kama maisha ya (? unga)
anajua aki*loss ‘atatumikishwa kama punda
ataishinda nafsi, ataepuka tamaa za ngono
miguu ndani ya (?) kesho anachukua kisomo
na mungu atabariki kazi za yake mikono
ataitafuta riziki, anajua haiji mpaka aifate
cha mwenzake sio chake, hawezi kukimezea mate
atauchukia muziki j*pokuwa ndio kazi ya babaake
studio, na shoo za usiku huwa zinamuudhi mamaake
anajua fika ‘hakuna jipya chini ya jua
hivyo atakufa, akitafuta ‘hawеzi kufa kwa ajili ya anasa
anamshangaa tajiri anamtoa mwanae kafara
ili ‘afanikiwe kibiashara
mwanadamu haridhiki ndio maana hajakamilika
[uwizi] wanaifua maiti, wanai*search kisha wanaizika
mwanangu anasita kuja duniani, dunia inamtisha
anasita, ‘kuja duniani, dunia inamtisha
ananiombеa dua, mashairi yageuke kivuli, babaake ali epuke jua
gari na nyumba nzuri kwa hii santuri ‘utayo pakua
nikishindwa ninunue mwamvuli ‘masika utakinga mvua
[chorus: banana zorro]
kila siku ndotoni
mwanangu ana nijia
kila siku ndotoni
mambo mengi ananiambia
kila siku ndotoni
mwanangu ana nijia
kila siku ndotoni
mambo mengi ananiambia
(instrumentals)
Random Song Lyrics :
- vado - slimesito lyrics
- sociedade dos poetas mortos - funkero lyrics
- suicide drive - adian coker lyrics
- younger (r&b mix) - jonas blue & hrvy lyrics
- ambitions of a rida - jgreen lyrics
- g.o.r. (god of rap) - lil b lyrics
- sexual lover - paulina rubio lyrics
- edge of destruction - dig_90 lyrics
- tarántula - lucas skillz lyrics
- stoję pod twoim domem - edzio lyrics