juhudi za wasiojiweza - fid q lyrics
[intro: bi. kidude]
[drop]
juhudi za wasiojiweza
juhudi za wasiojiweza
[verse 1: fid q]
huu moyo huficha siri
ambazo kwa macho huzioni
kwa kuwa ‘mi si mchoyo
nitakupa jambo jipya sikioni
fedha zao ni nyingi, nyingi zaidi ya akili zao
hawasikilizi shida zako za msingi, na wao wanazao
mn*z* haupandwi kwa ukucha
na mpanda ngazi, hushuka
kuteleza sio kuanguka, mbaya ukishindwa kunyanyuka
anaye fanya, hajui chochote
anaye jua hawezi fanya, ambaye amechoka kufikiria
au ana amini anajua sana
kama haujutii ya jana, na pia hauofii ya kesho
unaweza kuyapatia kimaisha, yeah ‘au kuyaotea
unataka kuchukiwa na mjinga? muambie akikosea
ukweli siku zote unapigwa pingu, uongo uzidi enea
wenye nia hawana nguvu, na wenye nguvu hawana nia
wana ridhika na moja, wanaogopa kutafuta mia
wanayafokea maji wakati wanaogelea
ukiwakosea ‘hawa press charges, vidole vyao vimeenea
uzembe umewafelisha wengi na bado wengi wanatega, wanaumia
hii dunia imewaangukia juu ya mabega
na wakilega, wanakosa hata food juu ya meza
sina budi kuwaeleza, hizi ndio juhudi za wasiojiweza
umewafelisha wengi, na bado wengi wanatega
wanaumia, hii dunia imewaangukia juu ya mabega
na wakilega, wanakosa hata food juu ya meza
sina budi ‘kuwaeleza, hizi ndio juhudi za wasiojiweza
[interlude: bi. kidude]
moyo nakuambia, tizama ukihisi
usicheze na nyonda, usiojua hufi
mzoea punda, hapandi farasi
hapandi farasi, kwake si mzuri
j*po (?) nguza (?)
huona najisi, si yake fahari
si yake fahari, kweli nakuambia
nguru kwa ugali, amezoea
ziwa kwa sukari, ukimpahulia
ukimpahulia, kasikitika
dodo hujitia, kayatapika
…
juhudi za wasiojiweza
[verse 2]
wanajifanya ‘w*n*leta misaada k*mbe waningiza madawa
[mtwara] tutakula wapi?
ndio kundi la kwanza kupagawa
wanatumia antidote kabla ya kuk*mbana na sumu
kuanzia unyayo hadi utosi, nje ndani, utajilaumu
hata dunia iki*change vipi, paka hawezi taga mayai
na ukiya chemsha, ukiya kaanga ‘haupati vifaranga, right?
wanamrudisha ndani ya maji samaki aliye kufa, afuf*ke
kamba iliyo legea, ‘kama una haraka usiivute
dini zinageuzwa kuwa biashara kubwa, kubwa, ‘huwezi amini
wanajaribu kutuangusha wanakuta tushalala chini
kuna maskini na omba omba, wanaogeuza kidonda mtaji
kuna ukimwi na siamini wagonjwa ndomu (?tumiagi)
anayezijua lugha tofauti, kote atapaona nyumbani
fanya uzijue na kona zote kama uf*gio wa zamani
amani ilileta pesa, pesa imeleta vita
hawazingati ‘mauzo ya wasanii baada ya kulipwa
ni vyema k*mpenda mkeo, siri zako umuambie mama ako
usije muonyesha utupu mkweo kisa umelewa, itakuwa aibu yako
mlevi kesho yake hujuta, zinapo mruka hana hata jiti
au labda alipigwa chupa, baa za siku hizi ugomvi wa viti
emcee mkali hushuka mzuka wa mistari kwa ubovu wa beat
au anapo rusha track kali, dj haipigi
“emcee mkali hushuka mzuka wa mistari kwa ubovu wa beat
au anapo rusha track kali, dj haipigi”
(instrumentals)
[outro: bi. kidude]
juhudi za wasiojiweza
…
juhudi za wasiojiweza
Random Song Lyrics :
- midnight rhymes - blueninja506 lyrics
- el indio enamorado - grupo laberinto & luis r conriquez lyrics
- bien guillao / calidad - uppermind lyrics
- gold star - cinnamontal lyrics
- winx open up your heart - winx club lyrics
- fieber - montez & sdp lyrics
- id pick up flowers - jake minch lyrics
- ange & démon - ratu$ (fra) lyrics
- слёзы (tears) - aquakey lyrics
- money! - rare americans lyrics