lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

usiku - duke & songa lyrics

Loading...

[verse 1: songa]
natoka bush, naingia dar
mataa yamejaa, kuona mw-ngaza naskia raha
nashuka kwenye ndinga naanza k-msaka uncle
nkilinda wajinga wasinpige changa la macho
nikamtafuta kila kona, haonekani
nkaingia kibanda cha simu, nikapiga simu hewani
samahani mteja unayempigia hapatikani
jaribu baadae, na kama ukishindwa hata mwakani
oh my god, ntafanya nini
wakati maskini na simjui yeyote hapa mjini
nkacheki mida, saa sita kasoro
pembeni nikaona giza, nkaanza kupita chochoro
vichaka vya ubungo, mashaka na mafumbo
mara nkasikia msaada vibaka wananipiga mtungo
sauti za chuki zikimfokea
nkasimama kutazama sauti inapo tokea

hook:
mi ni giza
kuna vingi vya kutisha
chunga sana pindi inapofika usiku
usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku
mi ni giza
kuna vingi vya kutisha
chunga sana pindi inapofika usiku
usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku

[verse 2: songa]
nikashtuka kuona njemba zimejipanga
wawili wamemshika binti mwingine amebeba panga
akili ikacheza usoni kijasho chembamba
huku nkiwaza kwa hizi njemba nitaweza tamba
bila kusita nikainama nikaokota mawe
kurusha nikampiga mmoja la kichwa, wacha apagawe
wawili wakakimbia, mmoja ndio akabaki
akataka tuanzishe vita sijui ana roho ya ki-gadaffi
nkaona poa, bila gumzo la kucheka
huyu bwege hanijui bush mi na tuzo ya mieleka
ngumi taekwondo hadi mafunzo yasiyo eleweka
pia nna ngumi kama nyundo huyu boya leo atabweka
nikarusha akakwepa, akarusha nikakwepa pia
nikamchota mtama, kuinuka akasepa na njia
kwakua ilikuwa giza, basi nikamwachia
akakimbia, huku binti akabaki -n-lia

hook:
mi ni giza
kuna vingi vya kutisha
chunga sana pindi inapofika usiku
usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku
mi ni giza
kuna vingi vya kutisha
chunga sana pindi inapofika usiku
usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku

[verse 3: songa]
nikamwambia binti usilie matatizo yapo
ila usiku kama huu kwanini unatembea peke yako
isitoshe we ni mrembo, upo shega balaa
kwa mavazi uliyovaa nahisi uliwatega jamaa
akasema, kwake huu ndio muda wa kazi
anauza mwili, ili apate mpunga wa malazi
nyumbani ana watoto
baba yao aliwakimbia, sababu ya wingi wa changamoto
anaganga na msoto
moto umetanda anashukuru j-po hawana kitanda ila ana ndoto
mara akaanza kulia eti kaka unaroho ngapi
nikamwambia usilie mi ndio songa nna roho safi
nakushauri sasa uende nyumbani
usiku usikukute hapa tena uende kwa amani
mshukuru sana mungu kwa kukupa usicho kiomba
kwa sasa naondoka zangu naenda k-mtafuta mjomba

hook:
mi ni giza
kuna vingi vya kutisha
chunga sana pindi inapofika usiku
usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku
mi ni giza
kuna vingi vya kutisha
chunga sana pindi inapofika usiku
usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...