siku mbaya - dizasta vina lyrics
artist : dizasta vina
song : siku mbaya
yeah!
black market!
ringle beatz!
nakurupuka kitandani baada ya ndoto za kutisha
moyo unadunda sana na jasho linanitiririka
macho nafikicha, taswira, naona kiza
kwa muda nasizi kimya na dakika zinapita
zikijirudia ndoto hatari naona woga
nakosa hoja napotafakari nilichoota
namwamsha wife aniwekee maji ya kuoga
ananijibu anahisi homa na mwili mzima umechoka
nampa pole, staki kuanzisha zogo wala nini
maana hata sura inaonesha ana kinyongo na mimi
ni muda sasa napokua nae hajiamini
nacheki saa nagundua nimechelewa kazini
napiga zangu maji mwilini
and just for the record, mimi ndo mtunza funguo za ofisini
nakuta wafanyakazi na bosi wapo getini
kwa ghadhabu kila mmoja akinitazama mimi
kabla sijameza mate wala sijabuni sala
naambiwa walikuja wazabuni kwa biashara
na kwakua nilichelewa kufungua ofisi
mchongo ukafa, nimeingizia kampuni hasara
baada ya masaa kibao ya kufikiri
ofisi ikaweka kikao kunijadili
waliniona driver nimeangusha basi
wakafikia mwafaka wakunif-kuza kazi
nikatahamaki, sikujua lakufanya
pale kwenye kamati hakuna wa k-mtazama
nikahisi ni mipango ya kikuda imefanywa
sio gari tu, maana hata nyumba nilinyang’anywa
nikajiuliza huruma imekwenda wapi?
kila mtu alijua kua nilipenda kazi
niliheshimu kama navyoheshimu ndoa ama mzazi
ama muumba, leo nimepata doa kwenye shati
acha familia, vipi deni la ofisi
wamenipa mwezi, nikifeli watanifilisi
mtoto shule, pia bunju nina shamba la kukopa
sijalipa na kijiji nina ndugu wa kutosha
nguvu zilimalizika, nikatoka kwa adabu
licha ya ghadhabu kunishika
nikajipa moyo kua nna mikono pia na miguu
vyote vyangu sina sababu ya kushindwa
nilikosa wa kunishika wa k-mweleza
mshahara ulikua mdogo nilishindwa kuwekeza
nikapiga moyo konde mimi mwanaume nita-fight
nikpanda gari nikampe taarifa wife
nikiwa ndani ya dimbwi la mawazo
nikitafakari hivi vitimbi na vikwazo
mbele yangu akakatiza mpita njia
kwakua sikua makini na gari nikamvamia
dakika mbili, wananchi wakalizunguka gari
wakinishutumu sana sababu ya mwendo mkali
nikaitikia wito nikitegemea thawabu
nikampeleka mgonjwa na akaanza matibabu
narudi zangu home, misemo ya kishenzi nikitema
chumbani nasikia mihemo ya mapenzi
bila hodi, mlango nikaufungua kwa ghadhabu
nikamkuta house-boy juu ya kifua cha mke w-ngu!
nikabaki kama zuzu
yule wa kunifariji ndio ameniletea uchungu
nilitaka nilianzishe sikua na nguvu
huku nafsi inanishauri kwamba nimwachie mungu
swalini kwamba sina moyo mkunjufu?
au kwakua muda sijaenda kuabudu?
au tuseme mja nina gundu?
au kwakua nilijenga nyumba na sikuwajulisha ndugu?
sijaona faida ya pato langu
wazazi walikufa bila kula jasho langu
mawazo kwenye kichwa yamezidi
dunia ina watu wengi na sioni wa kunifariji
naitazama ardhi, naitazama mbingu
sioni nuru nachoona ni maumivu
maswali mengi, bila majibu
ila swali kubwa ni vipi mimi nitaimaliza siku?
jua linazama bado sijiamini
naona nadondoka ila sioni nikifika chini
saa tano na dakika hamsini
bado dakika k-mi siku iishe na sijui kinafata nini
oh my god!
__________________________________________
Random Song Lyrics :
- seek & destroy (live at helping hands concert 2022) - metallica lyrics
- booti booti - stroppo lyrics
- rock me - fresh force crew lyrics
- werewolves (mordida) - lower mars lyrics
- рулетка (fr3 уже завтра в нули) - og buda lyrics
- 2024 man patinka taip gyvent, lietuvos balso mokytojų atidarymo šou - atlanta lyrics
- neighbours - aystar & mowgs lyrics
- endless torture - crucifiction lyrics
- en ung gadedigter - s4m1 lyrics
- mindset baby - ghosther lyrics