lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

not a hero - dizasta vina lyrics

Loading...

nikiwa narudi kutoka kwenye sherehe za mahafali
nikakatiza kwenye mtaa wenye taa mbali
kwahiyo giza kubwa nikiwa na tahadhari
huku nikitafakari

vipi maisha yatakuwa? shule nimeua naingia mtaani
je nitapata kazi au nitalamba nyasi?
au nitaingia shambani ama nitaishika gun?
mawazo kichwani kama nitaipata mali

mbele namwona lily, tunaenda njia moja
maana tunakaa mtaa mmoja, just kona mbili
bado alikuwa amevaa joho la kuhitimu
na mkononi simu, akibofya nini..

alitembea kulia kushoto, mwendo wa madaha
sometimes aruke kidogo kuonyesha furaha
aliyapiga majani kwa fimbo
nilisikia sauti kwa mbali akiimba wimbo

nilitamani k*mwita niliogopa
nilibaki nyuma nilizuga sik*mkaribia
maana kitambo ninamjua ila daily tu navunga
vile mazoea hatuna na namf*gilia

haikutokea siku, nidiriki kuthubutu hata
k*mfata k*mwomba contacts
j*po tunajuana tulisoma sekondari
msingi na vidudu k*mfuata niliona woga
moyoni napiga kelele “come and save me”
nazama kwenye bahari hii ya mapenzi
pengine pia alinihusudu ila sikuwa kamili
pengine nilikuwa na nguvu ila sikuwa jasiri

aligundua kuwa, namfata kwa nyuma
aligeuka aliniangalia nikauchuna
alinipungia mkono niliupunga pia
lakini bado nilivunga sik*mkaribia

hofu iliufunika upendo w*ngu
kila nikimwaza yеye niliiwaza kesho yangu
nilitamani mrembo asimamе nimsemeshe soga
labda mikono tushikane tutembee pamoja

alikuwa karibu pia alikuwa mbali
nilijua kuwa naye penzini ingekuwa zali
nilitamani k*mfata nimweleza nilichowaza
nilishindwa ’cause…

(i’m not a superhero)
ile haikuwa filamu so, i was not (a hero)
ushujaa ni dhahania uhalisia hauna (hero)
(yeah yeah yeah, i’m not a superhero)
(yeah yeah yeah)
alitembea mbele nilibaki nyuma
mimi na moyo w*ngu mpweke uliojaa ufa
nikifurahia jinsi asili ilivyomuumba
nikijua dhahiri hofu haitazaa tunda

niki*fantasize siku atakuwa w*ngu
nikiomba mizimu ya mapenzi isikie dua zangu
na baridi ilinipiga ila haikufua dafu
nilikuwa mkavu

nilizidiwa na mawazo hisia nilikuwa nazo moyoni tele
masomo tumemaliza nitakuwa simwoni daily
mawazo nilipoyarudisha ndipo hofu ikanishika
niligundua malaika yule simwoni mbele

sikusogea karibu nilishapagawa
hisia ziliniambia kuna kitu hakikuwa sawa
nikasikia purukushani nikaingiwa hofu
nikavamia karakana chini ya gari bovu

nikajificha

nikaona vijana wamefura dhambi
mkononi mapanga usoni wamekula maski
wakamwingiza lily kwenye karakana
hawamk*mvua nguo zake walizichanachana
nilimwona lily, lily aliniona mimi
tukagonganisha macho ila sikutoka chini
akijua kuwa nina mpango wa k*msaidia
niliogopa nikamvungia akaanza kulia

maninja walimbaka mmoja mmoja
wakigombea kuanza hawakutaka ngoja ngoja
nilitamani muda urudi nimsemeshe soga
labda asingevamiwa kama tungekuwa pamoja

akipiga kelele “come and save me”
sauti yangu hata kutoka tu haiwezi
pengine yale yalinihusu ila sikuwa kamili
pengine nilikuwa na nguvu ila sikuwa jasiri

alininyooshea mkono sikuunyoosha pia
alitamani nitoke niende kusaidia
hofu iliufunika upendo w*ngu
nilipoyaona mapanga niliiwaza kesho yangu

alikuwa karibu, ila alikuwa mbali
kutoka k*mwokoa pengine ingekuwa zali
nilitamani k*mfata nimwondoe kwenye mkasa
nilishindwa ’cause

(i’m not a superhero)
ile haikuwa filamu so, i was not (a hero)
ushujaa ni dhahania uhalisia hauna (hero)
(yeah yeah yeah, i’m not a superhero)
(yeah yeah yeah)

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...