lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

nobody is safe 3 - dizasta vina lyrics

Loading...

ah
eyo kutoka panorama nasuk*ma ringi kisomi
maana wa kufanya hivi simuoni
na maji ni ya shingo nawapalia madingi kooni
kwa mistari mingi kushinda hata nzi sokoni

dizasta ndo’jina logo ya mtaa ina*shine kuta
na*type lugha usongo kushinda mdai fuba
nuksi kama asili iliyo*design kufa
shwain kaa kando uone game nai*define upya, yoh!

na usawa ndo’ huu sikosei
mnapotea kwa sababu hamna basics, na hapo ndo’mnayumba
ndio maana mkienda juu siongei na vikundi vyenu utafikiri
crew za ma*g*y, ski’za

mfumo wa nguzo za hizi tungo ni ishara kwamba nimefuzu
kwa maana hii miruko ni imara
niko sky natafuta kikomo, kwenye kisomo
nachora beyond normal muulize dubo dibala

expansion to the hypersp*ce
nakaanga mawe yanaiva ma*verse
unaweza ‘dhania ni complex ngwair ama utadhania langa rebirth
material deep huku diver haendi

ni kama mufti aliyelamba haramu
tumeganda hata kope haiyumbi utasema ameganda sanamu
sipo kwenye route ya wavuvi mamluki nipo na mafundi
kina ngugi wanawapa salamu

ukifika uliza utaambiwa mimi ni nani
utaonyeshwa mtiti kilo nyingi haipimi mizani
ukishindwa ita wabishi waje wahiji imani
waeleze naurudisha mziki nyumbani

na kama ndo’ unafika sasa karibu center ya tenzi, huh!
uone bidhaa bila ya expire date
kubwa kushinda hata empire state
so my single line is like your entire verse, n*gga

usinishike mkono nikipake
hatuhitaji shobo, ni vina na mishono ka zuria
tofauti na midosho ya kipambe
tofauti na ngono au drama za domo na wenzake

nishavunja mwamba kaskazini
tanzania hakuna mroma mwenye stamina ya ku*rap na mimi
mizuka hewani utadhani anaye*rap ni jini
nusu mtu nusu rap machine

najua ushasikia tenzi bro ebwana utenzi huu noma
ita wanafunzi waje waperuzi ngoma
we don’t play good ukija tuna*execute
ujuzi kama sherryl woods naandika zaidi ya daily news soma

panda safina imefunguliwa mito
na kingo ni mbovu ukioga tu umefunguliwa mito
wenzio wameacha mtindo wa kunichukulia simple
sikudanganyi hamna hewa huku nilipo

kwa maana ni juu sana hata ukibebwa kusogea bado
kwa hisia za ushairi napotea angani
kama vile jangwani zinavyopotea nyayo
ah! pesa inaongea nami naongea nayo

single nzito utafikiri na*double
nafoka kwa roho mbaya kama dingi wa kambo
muulize fifi niko real kiasi sili na sharo
ripoti kutoka kilele cha ubora kilimanjaro

ngoja tu*diverge, thanks to rap i won’t die virgin
mwandiko utasema kau*design shorty
sura ya kazi utahisi mdai kodi
rai ya uhai mashakani siku hizi emcees hawakai road

maliasili mama’angu anailinda kama mtoto wa majini
un*z*amini ndoto? mi’ni kwa mama’ako
ndoto kwa demu wako, hata baba’ako anatamani
kuwa na mtoto kama mimi

sahau kuhusu chips kwenye foil
hiki chakula cha ubongo cha ku*feed kids
kwa lugha ya ku*twist kama coil
na maisha yangu myth mpaka naenda deep unaweza hisi nai*discover oil

code zinafanya wazungu wanazunguka
mafungu wanafunguka, mazuzu wanazuzuka
nilikuwa mtupu nikaokota buku nikabukuka
leo nasimulia tungo tukufu ni ka lufufu kafuf*ka

legend kama koffi olomide
naikamata dar kama daudi wa kolomije
nawalaza doro si*follow bata na*follow mishe
na ufundi ni controverse utasema apollo mission

misele hapa mjini
natembea na begi la maiti nachinja bila kwere wala nini
busara tele utasema nyerere ama mwinyi
nafika kilele ila sipigi kelele kama nyinyi

fuvu limeshiba mautundu kwenye kichwa
niko underground na huku ndio mitutu inakofichwa
walikuja na gubu walizikwa kama wafu mbongo tubu
wazungu wanasujudu hiki kichwa

we ni player unasifika? mi’ ni game
kitambo kama zinja kwenye plane za afrika nasikitika hamjui
messages n’nazo*pack kwenye pictures n’nazo paint
niki*reveal scriptures kama saint uh!

ni kama big hulk kwenye mini*bus
sitoshi kwenye skinny vazi
gani lita*fit, ma*emcee wana*sound kama injini yenye hitilafu
mi’ni king wa swahili rap get’t? (yeeah!!)

wanasema i am too real for the industry
stockhom mpaka italy
ka’ cruise yatch, groove hii ni concord
focus kama msongo ama mnoko anaye*solve murder mystery

(ama’ g.o.a.t you can see that) look at my family tree
look at the chemistry i have, look at my pedigree
you talk about being competitive? being authentic or
having body of work or longevity?

cheki hizi rythms cheki silabi
wananiita trickster cheki ma*trickery
ma*emotions passion love hope sympathy
uh! utahisi mkono wa mungu umeandika hii

na*spit holly ka’ n’nam*bite masihi
kwa heshima namnyang’anganya mic madee
hii ni fact hakuna emcee wa ku*rhyme ka’ d
shorwebwenzi nenda uka*bite na hii

ni deep sana na ndio maana wanaita ngumu ku*rap
deep kama chumvi kwenye uvungu wa ny@p
kabla hujani*book nitoe kwenye hayo mafungu pumbavu
mi’ sio malaika mi’ ni mungu wa rap

haleluyah!

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...