moyo - dizasta vina lyrics
verse i
tamaa ya mwili ikichukua nafasi..nafsi inasita na moyo huwa unadunda kwa kasi…moyo dhaifu hutekwa na dhambi… huku viungo hugeuka mtumwa na ndio maana hutenda kila kazi…
kazi inapokwisha nafsi inasuta…majonzi hutawala uso na huku moyo unajuta…moyo ukizidiwa wengi husema kwa wenzao…kutafuta nafuu na wengine uzitoa nafsi zao…
dunia imejaa choyo na dhiki…ewe rafiki k-mudu inahitaji mioyo thabiti… hatujifunzi kuwa na mioyo dadisi… maana tunakata tamaa kwakuwa tuna mioyo rahisi…
kuna kupenda nje na kupenda ndani…ndio tofauti ya moyo wa kupenda na kutamani…moyo wa urafiki una husuda… ila moyo mnafiki…umejaa unafiki ka
ma yuda..
moyo wa asiye ogopa huufata usawa wake… moyo wa ndege mwoga ndo uzipiga mbawa zake…mizimu itaishi bila moyo mpaka lini… siri ya mtungi ni kata je siri ya moyo ni nini??
verse ii
ni kama mc alivyo na moyo kwenye fani…yaani anashindwa na bado ana moyo wa ushindani…au mkristo alivyo na moyo wa imani…ya kuwa yesu atarudi na siku haijulikani…
kuna binadamu wana mioyo ya mbwa mwitu…yaani wamejaa ukatili mfano wa simba kwenye msitu…nahisi mapenzi kwenye moyo wenye wivu…heri mwenye moyo safj maana ndo ataiona mbingu…
moyo wa ushirikiano moyo wa ushirikina…moyo wa ugombanishi ndio moyo wa fitina…moyo wa kuweza moyo wa kuhisi ka unaweza…moyo wa majivuno ndo ujikweza…
natamani macho ya roho nione uso wa mwongo…moyo ulioshindwa ndo huamini nguzo ni hongo…moyo ni fumbo kwa watoto…ukifa moyo unabaki ubongo wenye lundo la misongo (ya mawazo)…
utashindwa ukiwa na moyo wa bandia…k-mbuka haufiki mbali bila moyo wa nia…kama ukikata shauri unga mkono na mimi…siri ya mtungi ni kata je siri ya moyo ni nini??
verse iii
fumbo ni mfupa kwa kibogoyo…hoja juu ya kiki ya mujwahuki kiki inayodunda kama moyo…moyo wa upole ndio moyo wa mke kwetu…tulia kwa bwana moyo w-ngu sifa mpe yesu…
naona moyo wenye kona…eeh maana kigeugeu utadhani moyo wa kinyonga…nna maarifa sina choyo so nabonga…unaweza kuwa na roho ila bila moyo hutasonga…
bila ya moyo vipi utaficha michongo yako??…ndo ujue ukubwa wa siri ndo ukubwa wa moyo wako…una uvumilivu?? tutajua… pale tutapogundua mimba unayolea mtoto si wako…
sera bubu tungejua…. viongozi wadokozi tusingethubutu kuwachagua…moyo unamengi inafika hatua ….
kichwa kidata raia zinashindwa kuamua…
moyo wa shobo si unapenda?…sio kweli kuwa mpenda ndogo ndo ana moyo wa kipemba… usipo uelewa moyo utanielewa mimi…siri ya mtungi ni kata je siri ya moyo ni nini?
Random Song Lyrics :
- im here - juice wrld ft xxxtentacion & lil peep lyrics
- pryachu lico - viceset lyrics
- sexo en el oxxo - vete ala versh lyrics
- eu to chique - lil on3 lyrics
- wallflower - goldfinger lyrics
- кризис (a crisis) - kasudoza (касудоза) lyrics
- le film - zed yun pavarotti lyrics
- arable shots - crops lyrics
- blockgeschichten - lighteye beatz lyrics
- skoda - moglii & lissa lyrics