lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

kikaoni - dizasta vina lyrics

Loading...

najivunia kulala na mkeo
nimevumilia sana na leo
nimeamua kusema sijali ka’ utanikaba koromeo
utanivunja na kuniacha kimeo…
kamwe sijutii katu

sijutii katu
piga kelele jaza umati sihofii watu
nimekubuhu mpaka inafika hatua
nimefanya mtaa mzima wanajua
nasifikirii ni rafu

kwa mitindo zaidi ya saba
na maumbile nimejariwa si haba
nilimpa raha kote kwenye gari na valanda kama mfungwa aliyekutana na kahaba

ona mrume ndago bila kiwewe
kila uliposafiri mi nilipiga misele
aliponiita niliitika kuzizima kelele
na nilipofika nilihakikisha anafika kilele
alinipeleka mbali kwa misemo motomoto

hadithi njoo utamu kolea
ukihisi naongeza chumvi kwa maneno ya uwongo ona alama ya meno kwenye mgongo alafu ngojea

ni hakika alinik-mbuka kila mida
na aliponihitaji niliibuka bila shida
alipopata swali aliniona mimi kwanza
akajiita jenny nikajiita tarzan believe that?
alifika alikaza na kamba
aliweka mizizi ya kukata na panga
alichizika utasema mwehu
moyoni aliacha alama ka ronaldo alivyoacha alama bernabeu

nilikuwa siufahamu ugoni
ah
kama kufumaniwa ni dhambi na nitapata adhabu motoni
nitaenda na tabasamu usoni

labda wakati ni sasa nimerudi kuenzi nafasi
napenda uhakika silengi bahati
naomba ujue kuwa mkeo mkeo hakupendi kwa dhati
k-mlazimisha ni k-muezi hayati

sasa kwanini usinipige na ulivyojifugia misuli
nivunje mbavu zangu labda utajisikia vizuri
fanya maamuzi sasa maana najitia kiburi
niue leo walimwengu wataf-kia kaburi

najisikia uchovu na mihayo napiga
uliza hizi nyayo na nyika
nimetoka mbali fanya maamuzi tuhitimishe kikao
maana hata mimi nina mishe kibao

mishe hata wewe unazo mishe unazobadili
fafanua eleza na uweke mifano isawiri
huo ubishi kujikweza weka kando ukatili
leo ndio mwisho vinavunja ndoa yako batili
andika talaka ili tuondoke

maana maamuzi ni yako au chukua panga unichome
haukuitendea haki kura yako
kuchagua ndoa wakati sio jambo kubwa kwako
utakapo chukua wasaa utagundua ulimpa saa alipohitaji muda wako

anajua kuwa mkoa wa mbali una watoto
anajua kuhusu vikao na safari za uongo
anajua kuhusu kondomu ulizobana kwenye nguo
na meseje za wasichana wa chuo. (sniffs)

ulimkuta mwema ukamteka kiakili
ukamshawishi mpaka akakupa shehena ya mwili
akakupa moyo akihisi utaweka nadhiri
ukajisahau na k-mwonesha asili
ya kwamba wewe ni mchafu tu

kipi unalopoka lakini?
ubaya ulipokuwa ubaya unachokonda ni nini?
mmoja amatupa mwingine ameokata yamkini
aliyetupa ni wewe na aliyeokota ni mimi. ah!!

ilikuwa sababu ya msongo wa mawazo
ndio maana uliona wife sio wa moto kama mwanzo
aliteseka kiasi alihisi ndoa ni sumu
na nikachukua maamuzi magumu
dongo kwako

nilimwokoa na nikamvusha bahari
maana muugwana vitendo maneno hayataangusha jabali
siku mwili hautagusa sayari
utamk-mbuka na pengine utajifunza kujali

mpunga umeyumba umeanza kujishuku mzee
umerudi nyumbani baada ya kushindwa k-mudu starehe
haukuwepo kwenye shida ilipofuzu tarehe
ulikimbia na nilikuepo mimi pekee

ngoja nikuudhi unajua mwanao ananiita daddy
nampeleka shule namrudisha nyumbani baada ya kazi
nalipa ada, ada usizok-mbuka kutoa
mwanao amefikia barehe na nimemfunza kunyoa
nimemfunza ushahiri nimefumfunza kufanya mahesabu
nimemfunza kufunga tai kisha kamba za viatu
nimemfunza sheria zinazoongelewa bungeni
na nilienda k-mtetea alipoonewa shuleni

unahoja yoyote defensively
maana haujui kama w-n-lala na kuamka safely
haujui kuhusu family dinner
woman’ s day, birthday zao haujui hata anniversary

haujui maumivu aliyoyapata moyoni
haujui harufu ya chakula alichopasha jikoni
haujui kuhusu depression maana mara mbili nimemkuta amejifunga kamba shingoni…

nampenda yeye amenifanya nipate ishara
amenipa counselling amenifanya niache sigara
anajua chakula nipendacho timu niipendayo kinywaji anajua even my favorite colour

wenzio tunatafuta familia ili tujenge wewe yako ni lini?
mkeo amesaliti ndoa sababu yake ni upweke sababu yako ni nini?

you know what they say… what goes around comes around man
yeah thus true… so i wonder why you changed you use to be a good man
what happened to you?

nakiri mbele za watu nilishiriki hii dhambi
uvungu wa moyo w-ngu unasema usaliti ni haki…
nyajua kisu chako uniue ila naomba uelewe
sijavunja ndoa yako umeivunja ndoa yako mwenyewe
aah

edited by benix matrix
©panoramaauthentik™

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...