lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

fanani - dizasta vina lyrics

Loading...

“talent and ability, can take you to the top of the mountain. lakini, the moment you mess up with your character, everything goes back to zero. unaanguka chini kabisa”

natembea sehemu nyingi nakutana na
watu wengi wananipa ushauri mwingi
mwingi mwingi blah blah blah
mbona hau*move hivi
mbona sijui hau*force kingi
mbona sijui hau*change hiki blah blah
fanya collabo na flani na flani blah blah
ule wimbo sijui ungemweka flani blah blah
flani na flani sijui hawawezi fani, flani sijui hamjui flani
flani sijui yuko kama flani blah blah

mchumba anahisi nauza bangi
anashangaa nimesoma sijatafuta kazi
namwambia mistari yangu ni bidhaa
nimelelewa vyema na sasa na sasa nailea hii mitaa

mitaa inahisi nauza pakti
nimechoka naunga waya naunga nyagi
mwonekano nje hauonyeshi nina kisomo
eti ubaya wa cover ndo’ yaliyomo

mama ana*wish nimwoe tuntu
anasema amesoma anamjua mungu
namwambia “tuntu anawadharau ndugu”
“na anaona mafanikio ni kupata bwana mzungu”
mama tuntu anasema mi muhuni
anahisi nipo ghetto n*z*enzi kunguni
haamini naheshimika kwa kuuеnzi utamaduni
ana anahisi muziki dhambi kwahiyo siendi hata mbinguni

hajui kuwa imani yake ni dau pana
la mchungaji, anahisi mi’ mdhambi dharau sana
nawa*overatе watu nasahau kwamba
people with common sense mtaani are outnumbered

mama anasema nabonga hanielewi
nimezongwa siwezi kutoka na sihemi
natembea na makaratasi utadhania mkandarasi
sina ganji utahisi nimerogwa na washenzi

namwambia “ujuzi power” nauhakiki
nimenawa mpaka naenda sawa na wahandisi
wauguzi wanapagawa wakifika himaya hizi
kuona sina dawa utadhania mvuta kaya chizi

mdogo w*ngu ana*doubt mi ni star
na anashangaa kwanini i don’t have a car
washkaji daily wanataka tupige picha
au short video intro tukazitundike insta

chuki nikiwaambia niko busy
hawaamini i have meetings to attend to
wanahisi nawadanganya wakaulize
kwani life is more than just instagram and facebook
wanasema mi’ kituko naruka luksi
nishatengwa na milupo ila sikugeuka nuksi
nilitishiwa hadi vifungo sikutupa ujuzi
utotoni sikupewa maputo niliokota books

sikupendwa na mazoba wakereketwa
ni’shaibiwa na manyoka na ndio maana niko focus
najua mikataba bogus inavyowateteresha
ndo’ maana huwezi kuona ninapelekeshwa

naakutana na
watu wengi wananipa ushauri mwingi
mwingi mwingi blah blah blah
mbona hau*move hivi
mbona sijui hau*force kingi
mbona sijui hau*change hiki blah blah
fanya collabo na flani na flani blah blah
ule wimbo sijui ungemweka flani blah blah
flani na flani sijui hawawezi fani, flani sijui hamjui flani
flani sijui yuko kama flani blah blah

hauwezi ku*observe my position, my momentum
at the same time? that’s cynical
i’m electron, i know how to move better, kunidharau
ni kuidharau uncertainity principle
naona wanaibuka wanariadha
wanafoka eti siongelei siasa
sijabuma, najua mchezo, ni kwamba
najua kukaa nyuma mbele masihara yakianza

life is when things happen so, let it be
we learn how to behave from the same sh*t
ninajua hizo struggle for revolution
and i knew it was time for change, so i change me

masihara ni fashion ukihitaji ule
hata vioo vya jamii vipo ndani mule
wasanii wanatumia style yangu bure
serikali hainitambui na ushairi w*ngu shule

mitaani juu hela haishikiki
nime*master mpaka school vyema hainishindi
sina matatuu natembea kwa miguu wananishangaa
i’m getting too famous for this sh*t

i’m a big deal nasahau sahau bwana
ila industry haiko real jau jau sana
maudhui ni kitu wadau walikacha
na maniga walisahau kuhusu culture
kisa njaa kubwa

mngekuwa wapi bila hiphop?
mngeshika wapi hizo dough bila hiphop?
mngekuwa wapi mapresenta wabovu
makundi ya matozi na hizi afternoon shows
bila hiphop?

ni vile ubishi nakazia
hawaelewi kazi yangu maana dhiki imen’dandia
mchumba n’nayembambia hasadiki nikimwambia
mi’ mwanamziki bado anahisi namtania

anasema namletea msongo wa mawazo
eti ooh! nimechoka na huo uongo wako
ana hofu that we don’t show off
go out and hit a club like a normal couple

kisa sija*fix my finances
she won’t fix her attitude
anafungua fridge yangu na hajachangia kitu
na anataka nimpeleke summer malibu

namwambia i have real life sio sci*fi
anahisi naishi honey boo boo lifestyle
oohh she wanna dance in the car
40 degrees she wanna shake her ass in a yatch

natembea sehemu nyingi nakutana na watu wengi
wananipa ushauri blah blah
mbona haumove hivi sijui mbona hau force kingi
mbona sijui hau…. blah blah blah
blah blah blah
blah blah
ushauri mwingi blah blah

man i’m outta here

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...