achia jala - dizasta vina lyrics
oya
mwela alikuja nikampiga sound mbumba mbaya
siwezi lala down town naitunza kaya
niko around ninavunja taya
michongo kibao town wana hawakuvuta waya
achia jala
ni heri kuyashinda majaribu
ila kufeli ni kushindwa kujaribu
baba alifeli siwezi feli pia
namiliki jina la ukoo sio sheli dia
siwezi lala njaa itanigaraza
kwahiyo usiniletee risala achia jala kwanza
sina kazi nimedandia ndala
alafu unanikazia fala
bro achia jala
hauna shida ndo’ maana unapendeza
alafu unaniambia hauna fedha
sikupi kichaka sikupi hata stata utakimbia
achia jala ntakupiga mitama utajifia
sikupenda kuwa vikundi vya wahuni
nilikuwa madini ambayo hauyakuti vitabuni
nilikuwa mtu kabla enzi zangu
haya maisha yangu ni kitabu na hii ni peji chafu
so achia jala
dingi mwenyewe alitoboka
madeni kama dhambi milele nakokota
na alipodondoka nikarithi shida
ndio maana kuelewa mtu lazima uelewe alipotoka
so, achia jala
sichezi kamali na washua
nitakupiga kabali nitakuua, sikuachii hata ukisali
matumaini yako mbali
nami nipo katikati ya bahari na mashua
hauwezi kuwa mtoto ukishazaa
nina mtoto sasa, sitaki kuuza ndoto ka bidhaa
mwanzo nilikuwa na ndoto na iling’aa
lakini bahati mbaya mtoto hawezi kula ndoto ikija njaa
nilipenda kuwa rubani
ila mambo ni makubwa ukubwani
nikaishia kuwa mkulima fani niliyofunzwa nyumbani
kabla shamba halijak*mbwa tufani
so achia jala
nimekufata tangu benki najua kuwa una cash
uliingia ukiwa empty ukatoka na mabegi
una*act kama ndezi
unaniletea undezi nitakuletea ushеnzi wewe
nilichora plan na sikupiga mchelе
wenzangu wa mtaani ni’shazika tele
najua unahesabu time si ujaribu kurun sijui
nimeshika gun nitakuchezea shere
achia jala
siwezi kudanganya kuhusu
haya madusko hatuwezi kugawana nusu
usihubiri sisadiki maadili
maisha yenyewe mafupi na hatuishi mara mbili
achia jala
mbunge halijui jina langu
ramani ya jiji haisanifu njia zangu
hawajivunii ndugu zangu, miungu haisikii sauti yangu
niko peke yangu mimi na gun yangu
nitaku pah pah
kisha unione mamluki
nitakuchezesha mabuzuki
nishafungwa mara tatu nimetoa roho nne
utakuwa wa tano, so jaribu kutoka nduki nikuonyeshe
nipo kazini so achia jala
nitakutia ngwara ufe
mafanikio ni kwa wale majasiri
walio tayari kusubiri ni makupe
nisikize brother
ni’shafanya mamziki
sikuvutia kukusanya mashabiki
naogopa kuwa begi nishazika marafiki
nilishalala na maiti nishajiuza kwa shangingi
nishafunga mahirizi, nishakula mamizizi
nishafuga jinamizi mamisuba nikasizi
nishakuzwa na waizi waliokuzwa na machizi waso….
mama ananiona failure for life
na ninamisi k*mbatio la wife
mkwe ananiona bwege, napeleka nuksi malangoni pake
shemeji ananiona sio type
so achia jala, nitakubia roho nipe jala
usinizoee usinipe gwara
unahisi sina maadili ninafata mk*mbo bwege
huwezi kuwa consious ukiwa tumbo empty
achia jala
sijarithi mali ili nizichunge kama zako
jala ziko mbali nizifuge kama zako
wajomba masadali sio wabunge kama wako
sijaenda shule yako…
i’ll f*cking shoot you, achia jala
nimeshindwa leo sio kwamba nilisinzia jana
sijakwambia kwamba alisinzia baba
hakujua mkwanja ni maua mazuri yanafifia ghafla
achia jala
hey, so sad hunijui boy, am not of your calibre
usituone tu tajiri, wengi tuna suck blood ki*cannibal
msimamo kitaliban, na roho ya kijahidina
kama mbwai mbwai ndio utajua mi kikosi kama pina
but i won’t choose that hata ka’ niko street smart
nna*pure fact nahisi we ni mgonjwa unahitaji meds
mental disturbed maybe afya ya akili
na uko so bitter it’s not healthy unapoteza asili
hata mi nilihaso man same thing na bakhresa
niliogopa pressure sikutafuta demu ilikua pesa
hata nikitesa,don’t judge me that’s my money
nyie waishiwa pesa mnatoaga advice kwani?
plus i got my family ambayo inanitegemea
na nasimama kama nguzo kwa nyumba wakiegemea
hata hapa umenisimamisha tu kuna muda unapotea
najua unapitia mitihani,ila kikubwa nitakuombea
bidii ni mazoezi tenda kwa muda uone matokeo
mafanikio yatakuja hakuna aliyezaliwa akiwa na cheo
ukipata wekeza ndio sababu sikupenda vileo
na kupunguza maninja ndio ueze k*mk*mbatia mkeo
nikutolee form twende huku kuna form
maisha kutafuta nilipo nilisepa home
blacks we don’t bend the knee ile ki uncle tom
upo kwa era wanaompenda ndio hawajui ku perfom
kuhusu muziki labda huku*appeal kwa soko poa
au whatever product ulitoa zilikuwa zinaboa
ulihitajika kuwa na strategy na market iliyobora
sio upate mchongo tu kisa ni kenwari bora wa kuchora
na usi blame wazazi kikubwa nikukuleta uhaini
unavyokua jambazi wana blame,wanini walizini
na kukupata wewe ambae una act mwewe,hufugiki
halafu skia kwanza haunitishi,nishaishi hata na mungiki
na kuua sio fani something u boss for
unajilaani damu mikononi and we both know
jiulize hizi roho ziliko zinamwambiaje mungu
na ubani unachomwa familia zikik*mbuka machungu
dogo sitakujenge leo twende tukajenge
we the first civilization mbona tufe kisenge
ukiacha jembe sahau kuhusu sembe
usinichanganye boy tukadhani mamba,k*mbe kenge
na kama wataka kuniua basi fanya fasta
ila k*mbuka nitakaowaacha hawatakuacha
sheria itakusaka na jela watakutupa
na utachacha,hautotoka miaka mpaka unakufa
sasa chagua nikusaidie kubadilika ama ubakie
na yote ulonambia nikusamee sitoyafikiria
unajua pia ni hatia tu kudhamiria kuua
ila i won’t press charge ukitaka kuacha na umeamua
najua hukushiba kwa ndonga walizokupa mtaani
oya mkali na hata hujui unaishi namna gani
haukimbizi shida kisa fake post kwa ig
kinachofanya sisters wanamegwa kabla id
it was all a dream kuna muda sikutaka kuamka
ndoto tamu hadi nikasahau kurauka
amka,kijana kuna shuka,yakutupa
shtuka ukiamka ukilala muhindi atakufungulia duka
pia mimi kuna muda nilikua hooker ka w*ngware
nilikua nakosa dish haki ya mungu hata kahawa ngware
boss hushika nare nikikosa leta ka kitu
and i lived with my young sis ye hutoka wera usiku
ila naamini opportunity comes in your working clothes
na subira huvuta kheri that’s a simple joke
tujifunze kujitegemea no pillars
hata bila bob,unaweza tu baki kama wailers
alafu juu ya bundles na vocha,hadi msosi unakosa
kisa kuparty,unarudi ghetto unakopa
mwenyewe unamkosa mwisho unapata broka
unaogopa,anakua player unapata coacher
you sound cool halafu yanki bado una future mbele
jiulize tungekua na taifa angekata tamaa nyerere
keep your hopes in the cloud boy unaweza kua cowboy
john were,be aware hufanani kua tough boy
hupati kitu leo (hupati kitu leo)
yeah! just change bro
you have a better future
i believe in you
start believin’
amani (wala siachii jala leo)
umekosa bro
siachii jala
no
Random Song Lyrics :
- ain't thinkin bout u - mile lyrics
- speed racer - ap tardi lyrics
- караван (caravan) - пикник (piknikband) lyrics
- vidas negras importam - martinho da vila lyrics
- santa claus is coming to town - angélina nava lyrics
- lonesome lane - gedeon lyrics
- dejalo atras - kynzo lyrics
- coffee vs. tea - harvey seasalt lyrics
- hit - baby lucka & chimichangas lyrics
- time - jorja smith lyrics