lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

a consfession of a mad man - dizasta vina lyrics

Loading...

ah nak*mbuka aliniambia akiniona mimi anaona upendo
anaona nchi ya ahadi anaona pepo
anaona future ya maisha anaona lengo
akiniangalia anaona kesho, n’kashangaa sana

she had her game tight
kwani licha ya aibu, alionyesha feeling that she can’t fight
alikuwa tayari hata kunipa game night
akiuliza “don’t you believe love in a first sight?”

nikamwambia “mbona una kasi ya jini?”
akacheka, akasema “brother wasi wa nini?” akideka
“we ni handsome, na pia ni mpole, mchizi ka’ wewe unahitaj manzi ka’ mimi” nikawaza…

alikuwa ana ‘summer body times two’
mi’ machoni nilimtamani ila ni nafsi tu
ndo’ inagoma akanishika sikio akanong’ona kwa mahaba akisema “dude i love you”

and then she called me names, mara ‘babes’
mara ‘boo boo’
akipitisha nails kwenye chuchu ah!
hata waungwana kwenye meza ya pembeni wakashangaa, wakauliza “d*mn bro una juju!?”

akataka anibusu n’kakataa kimtindo akanuna
akala mingo akanibusu kwenye shingo n’kaguna
akauliza “we umeoa?” nikasema “no”
“kwanini hunipendi!!?” nikasema “dada nakuonea huruma”
akahamaki “huruma ya nini boy!? una vibinti bar?
achana navyo ili niku*treat kama minister
hivi jinsi navyokupenda hauhisi raha? kwanini usikubali tuwe wote what’s so difficult?”

“unaonyesha walakini unan’shangaza
au pengine una ukimwi unaogopa kuusambaza?”
nikamwambia “sikia, najua kunielewa sio simple
mi’ nachinja watu nauza moyo na figo”
akacheka kwa mashauzi ya ‘kinafki’ ‘nafki’
ilikuwa ni wazi ali*doubt doubt
akasema “labda bro’ hauna kazi huh?
hiyo mioyo na figo ukichinja unauza wapi?”

nikamwambia “calls nyingi zinaingia
kila pande za nchi hizi pieces wan*z*via
mtandao unakua kila pande za jiji napopitia
na*expand treats mpaka india”

akacheka sana, mpaka akaniegemea
wakati peke yangu kichwani najisemea
“….dada angejua kitachokwenda k*mtokea
angebeba pochi yake angetembea, angekwenda mbali”

nikamwambia “nenda nyumbani usigeuke nyuma
kalale kesho nenda ibadani katoe ushuhuda
nakupa nafasi ya kuishi ipokee uujuze umma
kaandike k*mbuk*mbu kuwa umenusurika kufa”
akasema “sio mbaya nzi kufia kwenye kidonda
usiniache mimi maana nahofia kukonda
nakupenda sana please niweke moyoni hapo
ukiwa muuaji n’tafurahi kufa mikononi mwako”

hakutaka kusikia mambo mengi
kama bidhaa ameshailipia na sasa anasubiria “change”
kwa lugha ya nje ya dunia macho s*xy
akanikaribia kisha akani*kiss passionately, ah!

“do you have a car or some’ brother?”
translation akiuliza ka’ n’na gari labda
nilipomwambia mi’ muuaji aligoma
akaniambia twende home kisha akanidandia kifuani ghafla

ile nafsi bado inanikemea
najikuta peke yangu kichwani najisemea
“binti angejua kitachokwenda k*mtokea
angebeba pochi yake angetembea angekwenda mbali”

kivivu tukazama kwenye harrier
safari kwenda home bila barrier
baada ya nusu nikampa mvinyo wa baridi wa kiitalia
na ndani yake nikaweka valium

akapiga fundo kisha akaweka glasi mezani
akatabasamu akasogea hadi jirani
akaweka mkono wake begani
kisha kiudadisi akaniuliza honey hujaniambia
unafanya kazi gani
nikamuonyesha picha za mademu kama mia
niliowachora akasema “baby we’ ni g*nius”
nikamwambia “niliowachora nishawachinja you’re the next one” akasema “baby haupo serious”

aliniimbia wimbo maneno yakikata kinywani
ishara ya kwamba kimtindo dawa imeshapanda kichwani
nikambeba kisha nikampeleka mpaka chumbani
hakukuwa na kitanda zaidi ya meza nikamlaza mezani

nikamchora, nikimtizama mwili wake wa mvuto
huki nikiwaza “unapopenda ukubali majuto”
nikampiga busu zito kwenye paji la uso
kisha nikatoa visu vikali na nyundo

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...