lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

niambie - benkai lyrics

Loading...

[intro]
yeah, yeah yeah hii yeah
benkai, oh yeah

[verse 1]
kusema ukweli nakupenda ila vile kunaenda unanichanganya
kila wakati unanilenga nikitaka tukutane unanidanganya
hujui unanisulubu kwa wako moyo wa barafu
unaniwekaga roho juu unavyofanya sio sawa boo
kama umechoka basi nifahamu sije nikakosa raha
makosa kama ya kalamu tunaweza kuyafuta
afadhali nitulie
na moyo w*ngu mi niachie

[chorus]
niambie kama sikufai nifungashe virago
usinitese mie nikiumia moyo niseme wewe ndo chanzo
niambie kama sikufai nifungashe virago
usinitese mie nikiumia moyo niseme wewe ndo chanzo

[verse 2]
enzi za kudanganya danganya sitaki tena
na huba langu ushachana ukanipiga chenga
yaani wivu maumivu wadogo kwa wakubwa wakosa jibu
madhara ya moto majivu yanachoma sana yalinisibu
sitaki lijirudie jinamizi lakaba koo
afadhali nitulie angalau nipoze roho
nimepanda mchongoma kuushuka ndio ngoma
una tabia za sodoma we maji moto unanichoma
[outro]
ninakutaka uko wapi
nakuhitaji uko wapi
ninakupenda uko wapi
where are you now that i need you
ninakutaka uko wapi
nakuhitaji uko wapi
ninakupenda uko wapi
where are you now that i need you

[chorus]
niambie kama sikufai nifungashe virago
usinitese mie nikiumia moyo niseme wewe ndo chanzo
niambie kama sikufai nifungashe virago
usinitese mie nikiumia moyo niseme wewe ndo chanzo

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...