lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

maamuzi - bahati bukuku lyrics

Loading...

maamuzi yako matokeo ya kesho
amua vema upate mema wewe
maamuzi yako matokeo ya kesho

amua vema upate mema wewe

alikuwepo mama mmoja ngoja niseme
jina lake aliitwa tundo
alisumbuliwa na ugumba miaka mingi
ndoa yake ilikuwa matatani

hata mawifi zake wote hawak-mpenda tena
tundo aliamua kwenda kwa waganga
alizunguka huku na kule kutafuta msaada
aliona bora aende kwa waganga tundo

maamuzi yako matokeo ya kesho
amua vema upate mema wewe

alikutana na mganga mmoja nchini congo
akampa dawa za kutosha tundo
tundo alizaa mtoto wa kiume
jina lake alimwita sinona
maajabu aliyokuwa nayo mtoto yule
alikuwa amezaliwa na meno
maajabu aliyokuwa nayo sinona
alizaliwa n meno kama mtu mzima

tundo kwa kuchelewa kwake alifurahi
akaamini mganga amemsaidia
lakini alipokuwa akinyonyesha mtoto yule
ghafla alimng’ata mwili wake tundo

mwili ukapoa wote upande mmoja
lilikuwa ni tatizo lililomsumbua tundo

maamuzi yako matokeo ya kesho
amua vema upate mema wewe

tundo alilia akisema mwili w-ngu wote
sasa umebadilika
rangi ya ngozi yake tundo
iligeuka ikawa gamba la nyoka mwili mzima
siku moja marafiki zake
wakamtembelea tundo
siku moja ndugu zake
walipomtembelea tundo
wakalia sana wakamwambia ndugu yetu
tundo
tuna muhubiri anahubiri twende ukaombewe tundo

maamuzi yako matokeo ya kesho
amua vema upate mema wewe.
maamuzi yako unayochukua
amua vema upate mema

tundo akaondoka na mtoto wake
huku tatizo la utasa limekwisha
na kufurahia k-muona mtoto
alipokuwa muhubiri akihubiri
aliliona tundo mbele yake
akamwambia mama njoo mbele
tundo akasogea akijua muujiza umefika

akamwambia tundo njoo mbele
tundo akijua mungu amesikia

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...