mtazamo - afande sele lyrics
[verse 1: solo thang]
yeah…
yeah…
hakuna s bila o
l bila o
mwingine aitwe’ thang bila solo
shupavu’ awajibike kama apollo
jay, afande!
ni ukuta’ wapi uchochoro?
hakuna s bila o
l bila o
mwingine aitwe’ thang bila solo
shupavu’ awajibike kama apollo
jay, afande!
ni ukuta’ wapi uchochoro?
yo naghani’ ni mtazamo wa fani
ile dhana ni uhuni wameleta hawa katuni
kuna ku*rap na k*mbwata
ma*reaper na ma*rapper
katuni, tungo tata
wapi ulipo we jaku?
unakuwa mtumwa ili upewe promo kuuza
au kama ni binti’ ukalale kwa prodyuza
ma*promoter wana uma tu’ hawajui na kupuliza
na siku wakipuliza jua kidonda kishaoza
natamani kuwa huru mnyonyaji asinidhuru
wanaitwa “ma*emcee” hawajui mitindo huru
huu mtazamo w*ngu’ naona vingi vioja
yaani watangazaji sasa’ ndo ma meneja
vidato sita nlivyopitia
ndivyo vinavyonisaidia
mbunifu ukiizingatia
hata wakinibania
ni kipaji tu
ni mtazamo tu
msikasirike wash’kaji
haya mawazo tu
ulamaa…
[chorus: prof.jay]
ni mtazamo*zamo, mc’ usiogope kivuli
bora ukemee mabaya na usifie mazuri
ni mtazamo*zamo, mc’ usikwepe umande {dj scratching}
okoa sanaa ya bongo’ ili uchumi upande
ni mtazamo*zamo, mc’ usiogope kivuli
bora ukemee mabaya na usifie mazuri
ni mtazamo*zamo, mc’ usikwepe umande
ni ulamaa, professa jay, afande
[verse 2: prof jay]
ni mtazamo
rap inakuwa ni mikingamo
sasa watoto wadogo
wanajiita watu wa makamo
wanakwenda hatua mbili, wanarudi k*mi na kujipongeza
bila kuzingatia hatua nane walizopotеza
hao ni maf*kara wa akili zao’ na uwezo wao
wasio tambua nini na nini ni hatma zao
ma*gwiji vichwa chini, nadhani wanatunga sheria
lakini sheria msumеno’ isije ikawarudia
yes! ma* underground wanafanya rap inang’ara
lazima muwe vinara’ kwenye msafara
rap na mazingaombwe
habadani! haviendani!
msitegemee …“tawiree!” iwaokoe katika fani
ni vyema ukafikiri kabla ya kufanya maamuzi
tazama mbele’ usije ukanywa chai kwa mluzi {whistling}
na amini askari shupavu ni lazima upitie depo’
vinginevyo ndugu yangu utakuwa’ unapaka rangi upepo
kama unapata moja, kwanini usipate na mia?
hiyo inawezekana’ kwa wote mlio na nia
sioni sababu za msingi’ kuomba kwenye mitaa
kama una kipaji’ iweje ufe na njaa?
[chorus:]
ni mtazamo*zamo, mc’ usiogope kivuli
bora ukemee mabaya na usifie mazuri
ni mtazamo*zamo, mc’ usikwepe umande {dj scratching}
okoa sanaa ya bongo’ ili uchumi upande
ni mtazamo*zamo, mc’ usikwepe umande
bora ukemee mabaya na usifie mazuri
ni mtazamo*zamo, mc’ usikwepe umande
ni ulamaa, professa jay, afande
[verse 3: afande sele]
asante profesa jay, majani na ulamaa
mmegusa nnapo’pataka
name kwenye mtazamo’ na jambo nataka’ kuweka
maana kila kukicha ma*emcees wanaongezeka
nasema very nice!
yes! rap kama dhehebu
wingi wa wasanii’ inaonesha ni dini swafi
yaani imekubalika’ waumini tuko wengi’
lakini bado na shaka’ sij*pata uhakika
wote tumesadiki?
au wengine ni feki’ mmetumwa kama mamluki
manake hamna maana
maana mna rap na (?)
mistari imekosa vina’
yenye vina’ haina maana
na kila mnapokaa
mnapenda kusengenyana
mnapenda kutetana na’
mnapenda kulumbana
mimi naogopa sana’ kwa jinsi ninavyo elewa
mwishoni mtatukanana
ama inawezekana’ mwishoni mkaja chinjana
na wote tuna rap tuonekane’ hatuna maana
wapi ilipo taarabu? ilikuja kwa kishindo hata wagumu walishaihusudu
kwa ajili ya malumbano’ mwishoni ikafa kibudu
shabiki piga simu’ changia mawazo yako, ni nani tutamlaumu?
nani tumchune ngozi? prodyuza aliyerekodi?
ama labda dj anayeipiga kwenye kipindi?
wengi wanaipenda rap
j*po rap haiwapendi
waungwana’ wanaicha
wapumbavu hawa ambiliki
hivi kwani lazima tuwe wote wanamuziki?
mi nadhani ingetosha wengine mmbaki ushabiki
huu ni w*ngu mtazamo
masela’ msijenge chuki
{hata na majani}
[chorus]
ni mtazamo*zamo, mc’ usiogope kivuli
bora ukemee mabaya na usifie mazuri
ni mtazamo*zamo, mc’ usikwepe umande {dj scratching}
okoa sanaa ya bongo’ ili uchumi upande
ni mtazamo*zamo, mc’ usiogope kivuli
bora ukemee mabaya na usifie mazuri
ni mtazamo*zamo, mc usikwepe umande
ni ulamaa, professa jay, afande
Random Song Lyrics :
- bipolar rainbows - clarence clarity lyrics
- r.i.p. (remix) - dagarça lyrics
- stripped (terry urban remix) - duncan sheik lyrics
- twisted sheets - whitey lyrics
- girlfriend - max nasario lyrics
- milk and sugar - g. love & special sauce lyrics
- animal (spankers radio edit) - r.i.o. (germany) lyrics
- may i go to the bathroom? - chinese buddy lyrics
- spirit - doug e. fresh lyrics
- never young - gogol bordello lyrics