lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

nishike mkono - abiud misholi lyrics

Loading...

petero wa simon
alijaribu kupita juu ya maji kama yesu
alipoanza kuzama

kamwita yesu, nishike mkono yesu akamuokoa
wengine wanazama
wamekaa kimya na hali wanajua kwamba wazama
wengine wanazama
kwenye ulevi na hali wanajua wamekaa kimya
wengine wanazama
kwenye uchawi na hali wanajua wamekaa kimya
wengine wanazama
kwenye uzinzi na hali wanajua wamekaa kimya
wengine wanazama
kwenye magonjwa na hali wanajua wamekaa kimya

nasema, nishike mkono bwana
nishike mkono nishike mkono bwana nishike mkono
usiniache bwana
usiniache usiniache bwana usiniache
mimi ni wako bwana
mimi ni wako, mimi ni wako bwana mimi ni wako
wewe ni w*ngu bwana
wewe ni w*ngu, wewe ni w*ngu bwana wewe ni w*ngu
nakuabudu bwana
nakuabudu, nakuabudu bwana nakuabudu
usiniache bwana
usiniache usiniache bwana usiniache
beba mizigo yangu
beba mizigo, beba mizigo yangu beba mizigo
toa aibu yangu
toa aibu, toa aibu yangu toa aibu
lete heshima yangu
lete heshima, lete heshima yangu lete heshima

“unaponisikiliza saivi
natamani k*muona mungu anafanya kitu kwenye maisha yako
petro, alipiga kelele akasema yesu nishike mkono
nataka nikwambie neno moja kama petro angelinyamaza, hakika angezama
usizani ukikaa kimya katika hali ulionayo mungu atakuja mwenyewe kukutoa la hasha
katika wimbo huu nataka upanue kinywa chako umwambie yesu nishike mkono
umwambie yesu nitoe, bila wewe mimi siwezi
chukua hitaji lako likamate kwa mikono yako kwa imani
linyanyue juu katika kiti cha enzi
mwambie mungu nipo nakuabudu mahali hapa
mwambie bila wewe mimi siwezi
ndoa yangu haiwezi
watoto w*ngu hawawezi
maisha yangu hayawezi
wewe ndie msaada w*ngu
bwana nimekuja mbele zako sasa
niseme umwambie bwana nishike mkono
mwambie niko hapa nakuabudu, bwana atatenda kitu
halleluya
ohh, my god
naona neema ya bwana
naona uwepo wa bwana
naona maji ya uzima yanakusogelea saivi
ebu sema bila wewe siwezi”

bila wewe bwana
mimi siwezi, bila wewe bwana mimi siwezi
ndoa yangu bila wewe
mimi siwezi, bila wewe bwana mimi siwezi
watoto w*ngu bila wewe
mimi siwezi, bila wewe bwana mimi siwezi
hapa mbeya bila wewe
mimi siwezi, bila wewe bwana mimi siwezi
wapiga nondo wamejaa
mimi siwezi, bila wewe bwana mimi siwezi
bila wewe mfalme
mimi siwezi, bila wewe bwana mimi siwezi

“nataka nikuombee mama yangu
weka mkono kwenye tumbo lako
wakati naimba wimbo huu nimek*mbuka jambo moyo umeniuma
mama mmoja alipiga simu akasema anawatoto saba
nawote wanakula madawa ya kulenya
na wengine ni mashoga
yani anabeba mimba miezi tisa, anazaa shoga
anabeba tena anazaa mla madawa ya kulevya
akasema hakuna hata mtoto mmoja anayenisaidia
nataka nikuombee mama yangu sasa
maumivu ya watoto nayajua
weka mkono kwenye tumbo lako sasa
namuomba mungu saa hii, katika uzai wa tumbo lako
asitokee jambazi, asitokee kahaba, asitokee mtoto asiekuwa na adabu
mtoto aliejaa matusi
mungu akupe watoto wenye hekima
watoto wenye busara
wataompendeza mungu pamoja na wazazi wao
mungu akufute machozi, ufurahie uzao wa tumbo lako
ndo nimekuja mbele yako niendelee kuwalilia watanzania na kuwaombea
mungu awasaidie katika magumu mnayopitia
neema ya mungu ikufunike
neema ya mungu ikutetee
neema ya mungu ikuponye
bwana akupe haja ya moyo wako
akutangulie katika yote utakayotia mkono kuyafanya
neema ya mungu ikufunike
katika jina la yesu kristo, halleluyah”

we, nakuabudu bwana
nakuabudu, nakuabudu bwana nakuabudu
usiniache bwana
usiniache, usiniache bwana usiniache
mimi siwezi kwako
mimi siwezi, mimi siwezi bwana mimi siwezi
uniongoze bwana
uniongoze, uniongoze bwana uniongoze

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...